KIPINDI CHA 1 – MAISHA YA YESU
1. Jinsi Yote Ilivyoanza
1. Jinsi Yote Ilivyoanza
Luka 1
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 1
1Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. 2Waliyaandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona mambo hayo kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. 3Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, 4ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa.
5Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha ukuhani cha Abiya. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. 6Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama. 7Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana.
8Siku moja, ilipokuwa zamu yake kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu, 9Zakaria alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. 10Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani. 11Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. 12Zakaria alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13Lakini malaika akamwambia, “Zakaria, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. 14Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 15Atakuwa mkubwa mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. 16Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. 17Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama ya Elia. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake.”
18Zakaria akamwambia huyo malaika, “Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu.” 19Malaika akamjibu, “Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu; nimetumwa niseme nawe, nikuletee hizi habari njema. 20Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia.”
21Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakaria huku wakishangaa juu ya kukawia kwake hekaluni. 22Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu.
23Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani. 24Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema: 25“Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu.”
26Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27kwa msichana mmoja bikira aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu, ewe uliyejaliwa neema na Mungu! Bwana yuko nawe!”
29Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: Maneno hayo yanamaanisha nini? 30Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yesu. 32Yeye atakuwa mkubwa na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”
34Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. 36Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa. 37Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu.” 38Maria akasema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema.” Kisha yule malaika akaenda zake.
39Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yudea. 40Huko, aliingia katika nyumba ya Zakaria, akamsalimu Elisabeti. 41Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu, 42akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa. 43Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? 44Nakuambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha. 45Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokuambia.”
46Naye Maria akasema,
“Moyo wangu wamtukuza Bwana,
47roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu.
48Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu.
Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri.
49Kwa kuwa Mungu Mwenye Nguvu amenifanyia makuu,
jina lake ni takatifu.
50Huruma yake kwa watu wanaomcha
hudumu kizazi hata kizazi.
51Amefanya mambo makuu kwa mkono wake:
Amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
52amewashusha wenye nguvu kutoka viti vyao vya enzi,
akawakweza wanyenyekevu.
53Wenye njaa amewashibisha mema,
matajiri amewaondoa mikono mitupu.
54Amemsaidia Israeli mtumishi wake,
akikumbuka huruma yake,
55kama alivyowaahidia wazee wetu,
Abrahamu na wazawa wake hata milele.”
56Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.
57Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume. 58Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.
59Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria. 60Lakini mama yake akasema, “Sivyo, bali ataitwa Yohane.” 61Wakamwambia, “Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?” 62Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani. 63Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: “Yohane ndilo jina lake.” Wote wakastaajabu. 64Papo hapo, midomo na ulimi wake Zakaria vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. 65Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea. 66Wote waliosikia mambo hayo, waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: “Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?” Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye.
67Zakaria, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka unabii huu:
68“Atukuzwe Bwana Mungu wa Israeli,
kwani amewajia na kuwakomboa watu wake.
69Ametupatia Mwokozi shujaa,
mzawa wa Daudi mtumishi wake.
70Aliahidi hapo kale
kwa njia ya manabii wake watakatifu,
71kwamba atatuokoa mikononi mwa maadui zetu
na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72Alisema atawahurumia wazee wetu,
na kukumbuka agano lake takatifu.
73Alimwapia Abrahamu babu yetu,
kwamba atatujalia sisi
74tukombolewe mikononi mwa maadui zetu,
tupate kumtumikia bila hofu,
75tuwe wanyofu na waadilifu mbele yake,
siku zote za maisha yetu.
76Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu,
utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake;
77kuwatangazia watu kwamba wataokolewa
kwa kuondolewa dhambi zao.
78Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma.
Atatuchomozea mwanga kutoka juu,
79na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo,
aongoze hatua zetu katika njia ya amani.”
80Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionesha rasmi kwa watu wa Israeli.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
2. Kuzaliwa kwa Yesu
2. Kuzaliwa kwa Yesu
Mathayo 1:18-25, Luka 2:1-21, Yohane 1:1-18
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Mathayo 1:18-25
18 Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yosefu, lakini kabla hawajaishi pamoja, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 19 Yosefu, mchumba wake, kwa kuwa alikuwa mtu wa haki na hakutaka kumwaibisha hadharani, alikusudia kumwacha kwa siri.
20 Alipokuwa akifikiria hayo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto na kusema, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, kwa kuwa yeye atawaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”
22 Haya yote yalitendeka ili litimie neno la Bwana alilolisema kwa nabii:
23 “Tazama! Bikira atachukua mimba,
atazaa mtoto mwanamume,
na watamwita jina lake Imanueli”
(maana yake ni “Mungu pamoja nasi”).
24 Yosefu alipoamka usingizini, alifanya kama alivyoamriwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu awe mke wake.
25 Lakini hakumjua kimwili mpaka alipojifungua mwanawe wa kwanza, naye akamwita jina lake Yesu.
Luka 2:1-21
1 Wakati huo Kaisari Augusto alitoa amri ya kufanyika kwa sensa kote katika dola ya Kirumi. 2 (Hii ilikuwa sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Kirenio alipokuwa gavana wa Siria.). 3 Watu wote walikwenda kujiandikisha kila mmoja katika mji wake wa asili. 4 Hivyo Yosefu, kwa kuwa alikuwa wa ukoo wa Daudi, alisafiri kutoka Nazareti ya Galilaya hadi Bethlehemu ya Yudea, mji wa Daudi, ili kujiandikisha. 5 Alikwenda pamoja na Mariamu, aliyekuwa ameposwa naye na wakati huo alikuwa na mimba.
6 Walipokuwa huko, wakati wa kujifungua ukawadia, 7 naye akajifungua mwana wake wa kwanza, akamvika nguo za kitoto na kumlaza horini kwa sababu hapakuwa na nafasi kwao katika nyumba ya wageni.
8 Usiku huo walikuwako wachungaji katika mashamba ya karibu, wakilinda makundi yao ya kondoo. 9 Ghafla, malaika wa Bwana alitokea mbele yao, na utukufu wa Bwana ukawang’arimia pande zote; wakaogopa sana. 10 Lakini malaika akawaambia, “Msiogope! Tazama, nawapelekea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote. 11 Leo katika mji wa Daudi amezaliwa Mwokozi kwenu, ndiye Kristo Bwana. 12 Nanyi mtapata ishara hii: mtamkuta mtoto mchanga amefungwa nguo na amelazwa horini.”
13 Papo hapo pamoja na huyo malaika alionekana jeshi kubwa la mbinguni wakimsifu Mungu wakisema:
14 “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu anaowaridhia.”
15 Malaika waliporudi mbinguni, wale wachungaji wakaambiana, “Haya, twende mpaka Bethlehemu tukaone jambo hili lililotokea, ambalo Bwana ametujulisha.”
16 Wakaenda kwa haraka, wakamkuta Mariamu na Yosefu, pamoja na mtoto mchanga akiwa amelala horini. 17 Walipomwona, wakawaambia watu juu ya jambo hilo waliloambiwa kuhusu huyo mtoto. 18 Wote waliolisikia jambo hilo walishangaa sana juu ya maneno ya wachungaji. 19 Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo moyoni mwake, akayatafakari daima. 20 Wachungaji walirudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wameyasikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
21 Baada ya siku nane, mtoto alipokuwa anatahirishwa, aliitwa Yesu, jina alilopewa na malaika kabla hajatungwa mimba.
Yohane 1:1-18
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo Neno alikuwa kwa Mungu tangu mwanzo.
3 Vyote viliumbwa kwa njia yake, wala pasipo yeye hakikufanyika chochote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya wanadamu.
5 Nayo nuru hung’aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 Alikuja mtu aliyetumwa na Mungu, jina lake Yohana. 7 Huyo alikuja ili awe shahidi, ashuhudie ile nuru, ili kwa kupitia kwake wote wapate kuamini. 8 Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie ile nuru. 9 Kwani kulikuwa na nuru ya kweli, inayomwangazia kila mtu, akija ulimwenguni.
10 Alikuwako ulimwenguni, na kwa yeye ulimwengu ulifanyika, lakini ulimwengu haukumtambua. 11 Alikuja kwa walio wake, nao walio wake hawakumpokea. 12 Lakini wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. 13 Wao hawakuzaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.
14 Naye Neno akawa mwili, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
15 Yohana alitoa ushuhuda wake juu yake, akapaza sauti kusema, “Huyu ndiye yule niliyenena habari zake, ‘Yeye ajaye nyuma yangu amenitangulia kwa kuwa alikuwako kabla yangu.’”
16 Kwa maana katika wingi wa neema yake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 Kwa maana torati ilitolewa kwa kupitia Musa; neema na kweli zimekuja kwa njia ya Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana wa pekee aliye karibu sana na Baba, ndiye aliyemfunua.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
3. Utoto wa Yesu
3. Utoto wa Yesu
Luka 2:21-40, Mathayo 2:1-23
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 2:21-40
21 Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
22 Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana. 23 Katika sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.” 24 Pia walikwenda ili watoe sadaka: Hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana.
25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. 26 Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. 27 Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na sheria, 28 Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu, akisema:
29 “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. 30 Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu ulioleta, 31 ambao umeutayarisha uonekane na watu wote: 32 Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.”
33 Baba yake Yesu na mama yake walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. 34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; 35 na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako.”
36 Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. 37 Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana. 38 Saa hiyohiyo, alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu.
39 Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, wilayani Galilaya. 40 Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa naye.
Mathayo 2:1-23
Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu, 2 wakauliza, “Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.”
3 Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu. 4 Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”
5 Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:
6 ‘Ee Bethlehemu nchini Yudea, wewe si mdogo kamwe kati ya miji maarufu ya Yudea; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu, Israeli.’”
7 Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza wakati hasa ile nyota ilipowatokea. 8 Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.”
9 Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto. 10 Walipoiona hiyo nyota, walifurahi mno.11 Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: Dhahabu, ubani na manemane.
12 Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode; hivyo wakarudi makwao kwa njia nyingine.
13 Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.”
14 Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akaondoka usiku, akaenda Misri. 15 Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”
16 Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota walikuwa wamemhadaa, alikasirika sana. Akaamuru watoto wote wa kiume mjini Bethlehemu na kandokando yake wenye umri wa miaka miwili na chini yake wauawe. Alifanya hivyo kufuatana na muda aliopata kujua kutoka kwa wale wataalamu wa nyota.17 Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyosemwa kwa njia ya nabii Yeremia:
18 “Sauti imesikika huko Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumuua mtoto huyo wamekwisha kufa.”
21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea nchini Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
4. Maneno ya Kwanza ya Yesu
4. Maneno ya Kwanza ya Yesu
Luka 2:41-52
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 2:41-52
41 Wazazi wake walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki.
45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta.46 Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima.
48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.”
49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia.
51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake.
52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
5. Yohana Mbatizaji
5. Yohana Mbatizaji
Mathayo 3:1-12, Luka 3:1-3
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Mathayo 3:1-12
Siku zile Yohane Mbatizaji alitokea, akaanza kuhubiri katika jangwa la Yudea: 2 “Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” 3 Huyu Yohane ndiye yule ambaye nabii Isaya alinena juu yake aliposema: “Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’”
4 Yohane alivaa vazi lililoshonwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. 5 Basi, watu kutoka Yerusalemu, kutoka pande zote za Yudea na sehemu zote za kandokando ya mto Yordani, walimwendea, 6 wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.
7 Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja? 8 Onesheni kwa vitendo kwamba mmetubu. 9 Msifikiri na kujisemea, ‘Baba yetu ni Abrahamu!’ Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyafanya mawe haya yawe watoto wa Abrahamu. 10 Basi, shoka liko tayari kwenye mizizi ya miti; hivyo, kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni.
11 Mimi ninawabatizeni kwa maji kuonesha mmetubu. Lakini anayekuja baada yangu ana nguvu kuliko mimi, nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Yeye anashika mkononi chombo cha kupuria nafaka, ili aipure nafaka yake; akusanye ngano yake ghalani, na makapi ayachome kwa moto usiozimika.”
Luka 3:1-3
Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene, 2 na Anasi na Kayafa walikuwa makuhani wakuu. Wakati huo ndipo neno la Mungu lilipomjia Yohane mwana wa Zakaria, kule jangwani. 3 Basi, Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto Yordani. Akawa anahubiri watu watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
6. Magumu Katika Maisha ya Yesu
6. Magumu Katika Maisha ya Yesu
Isaya 53:2-3, Zaburi 69:7-12, Mathayo 13:55-57
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Isaya 53:2-3
Maana, mbele yake Mwenyezi-Mungu, mtumishi wake alikua kama mti mchanga, kama mzizi katika nchi kavu. Hakuwa na umbo wala sura ya kutupendeza, wala hakuwa na uzuri wowote wa kutuvutia.
3 Alidharauliwa na kukataliwa na watu, alikuwa mtu wa uchungu na huzuni. Alikuwa kama mtu kinyaa kwa watu; alidharauliwa na tukamwona si kitu.
Zaburi 69:7-12
7 Kwa ajili yako nimefedheheshwa, aibu imefunika uso wangu.
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu, kaka na dada zangu hawanitambui.
9 Upendo wangu kwa nyumba yako unanimaliza. Kashfa zote wanazokutolea wewe zimenipata mimi.
10 Nilipojinyenyekesha kwa kufunga, watu walinilaumu.
11 Nilipovaa vazi la gunia kuomboleza, wao walinidharau.
12 Watu wananisengenya mabarabarani; walevi wanatunga nyimbo juu yangu.
Mathayo 13:55-57
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi, amepata wapi haya yote?” 57 Basi, wakawa na mashaka naye.
Lakini Yesu akawaambia, “Nabii hakosi kuheshimiwa, isipokuwa katika nchi yake na nyumbani mwake!”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
7. Muujiza wa Kwanza wa Yesu Ulioandikwa
7. Muujiza wa Kwanza wa Yesu Ulioandikwa
Yohana 2:1-12
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Yohane 2:1-12
Siku ya tatu kulikuwa na harusi mjini Kana, mkoani Galilaya. Mama yake Yesu alikuwapo, 2 naye Yesu alikuwa amealikwa harusini pamoja na wanafunzi wake. 3 Divai ilipokwisha, mama yake akamwambia, “Hawana divai!”
4 Yesu akamjibu, “Mama, usiniambie la kufanya. Saa yangu bado.”
5 Hapo mama yake akawaambia watumishi, “Lolote atakalowaambieni, fanyeni.”
6 Hapo palikuwa na mitungi sita ya mawe, ambayo kila mmoja uliweza kuchukua kiasi cha madebe mawili au matatu. Ilikuwa imewekwa hapo kufuatana na desturi ya Kiyahudi ya kutawadha. 7 Yesu akawaambia, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Nao wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni mkampelekee mkuu wa karamu.”
9 Mkuu wa karamu alipoonja hayo maji, kumbe yalikuwa yamegeuka kuwa divai. Yeye hakujua ilikotoka, (lakini wale watumishi waliochota maji walijua). Mkuu wa karamu akamwita bwana arusi, 10akamwambia, “Kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakisha tosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa!”
11 Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.
12 Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
8. Kusafisha Hekalu
8. Kusafisha Hekalu
Yohane 2:12-25
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Yohane 2:12-25
12 Baada ya hayo, Yesu alishuka pamoja na mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake, wakaenda Kafarnaumu ambako walikaa kwa siku chache.
13 Sikukuu ya Wayahudi ya Pasaka ilikuwa imekaribia; hivyo Yesu akaenda juu Yerusalemu. 14 Basi, akawakuta mle hekaluni watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao. 15 Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazitawanya sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.. 16 Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!”
17 Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: “Upendo wangu kwa nyumba yako waniua.”
18 Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya mwujiza gani kuonesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
19 Yesu akawaambia, “Vunjeni hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu.”
20 Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arubaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?”21 Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya hekalu ambalo ni mwili wake. 22 Basi, alipofufuliwa kutoka kwa wafu, wanafunzi wake walikumbuka kwamba alikuwa amesema hayo, wakayaamini Maandiko Matakatifu na yale maneno ambayo Yesu alikuwa amesema.
23 Yesu alipokuwa Yerusalemu kwa sikukuu ya Pasaka, watu wengi walimwamini walipoona ishara alizofanya. 24 Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wote. 25 Hakuhitaji kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni mwao.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
9. Mtazamo wa Usiku Kumhusu Yesu
9. Mtazamo wa Usiku Kumhusu Yesu
Yohane 3:1-21
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Yohane 3:1-21
Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo. 2 Siku moja Nikodemo alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3 Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa tena hataweza kuuona ufalme wa Mungu.”
4 Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa tena!”
5 Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho. 7 Usistaajabu kwamba nimekuambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya.’ 8 Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
9 Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
10 Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israeli na huyajui mambo haya? 11 Kweli nakuambia, sisi twasema tunayoyajua na kushuhudia tuliyoyaona, lakini nyinyi hamkubali ujumbe wetu. 12 Ikiwa nimewaambieni mambo ya kidunia nanyi hamniamini, mtawezaje kuamini nikiwaambieni mambo ya mbinguni? 13 Hakuna mtu aliyepata kwenda juu mbinguni isipokuwa Mwana wa Mtu, ambaye ameshuka kutoka mbinguni. 14 “Kama vile Mose alivyomwinua juu nyoka wa shaba kule jangwani, naye Mwana wa Mtu atainuliwa juu vivyo hivyo, 15 ili kila anayemwamini awe na uhai wa milele.
16 Maana Mungu aliupenda ulimwengu hivi hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uhai wa milele. 17 Maana Mungu hakumtuma Mwanae ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali aukomboe.
18 “Anayemwamini Mwana hahukumiwi; asiyemwamini amekwisha hukumiwa, kwa sababu hakumwamini Mwana wa pekee wa Mungu. 19 Na hukumu yenyewe ndiyo hii: Mwanga umekuja ulimwenguni lakini watu wakapenda giza kuliko mwanga, kwani matendo yao ni maovu. 20 Kila mtu atendaye maovu anauchukia mwanga, wala haji kwenye mwanga, maana hapendi matendo yake maovu yamulikwe. 21 Lakini mwenye kuuzingatia ukweli huja kwenye mwanga, ili matendo yake yaonekane yametendwa kwa kumtii Mungu.”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
10. Mwanamke Kisimani
10. Mwanamke Kisimani
Yohane 4:1-42
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Yohane 4:1-42
Mafarisayo walisikia kwamba Yesu alikuwa anabatiza na kuwapata wanafunzi wengi kuliko Yohane. 2 (Lakini ukweli ni kwamba Yesu hakuwa anabatiza ila wanafunzi wake.). 3 Basi, Yesu aliposikia hayo, alitoka Yudea akarudi Galilaya;
4 na katika safari hiyo ilimbidi apitie Samaria. 5 Basi, akafika Sukari, mji mmoja wa Samaria, karibu na shamba ambalo Yakobo alikuwa amempa mwanawe, Yosefu. 6 Mahali hapo palikuwa na kisima cha Yakobo, naye Yesu, kutokana na uchovu wa safari, akaketi kando ya kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana. 7 Basi, mwanamke mmoja Msamaria akafika kuteka maji. Yesu akamwambia, “Nipatie maji ninywe.” 8 (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wamekwenda mjini kununua chakula.)
9 Lakini huyo mwanamke akamwambia, “Wewe ni Myahudi; mimi ni mwanamke Msamaria! Unawezaje kuniomba maji?” (Wayahudi hawakuwa na ushirikiano na Wasamaria katika matumizi ya vitu).
10 Yesu akamjibu, “Kama tu ungalijua zawadi ya Mungu na ni nani anayekuambia: ‘Nipatie maji ninywe,’ ungalikwisha mwomba, naye angekupa maji yenye uhai.”
11 Huyo mama akasema, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji, nacho kisima ni kirefu; utapata wapi maji yenye uhai? 12 Au, labda wewe wajifanya mkuu zaidi kuliko baba yetu Yakobo? Yeye alitupa sisi kisima hiki; na yeye mwenyewe, watoto wake na mifugo wake walikunywa maji ya kisima hiki.”
13 Yesu akamjibu, “Kila anayekunywa maji haya ataona kiu tena. 14 Lakini atakayekunywa maji nitakayompa mimi, hataona kiu milele. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji ya uhai na kumpatia uhai wa milele.”
15 Huyo mwanamke akamwambia, “Bwana, nipe maji hayo ili nisione kiu tena; na, nisije tena mpaka hapa kuteka maji.”
16 Yesu akamwambia, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”
17 “Huyo mwanamke akamwambia, “Mimi sina mume.” Yesu akamwambia, “Umesema kweli, kwamba huna mume.18 Maana umekuwa na waume watano, na huyo unayeishi naye sasa si mume wako. Hapo umesema kweli.”
19 Huyo Mwanamke akamwambia, “Bwana, naona ya kuwa wewe u nabii. 20 Babu zetu waliabudu juu ya mlima huu, lakini nyinyi mwasema kwamba mahali pa kumwabudia Mungu ni kule Yerusalemu.”
21 Yesu akamwambia, “Niamini; wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba juu ya mlima huu, wala kule Yerusalemu. 22 Nyinyi Wasamaria mnamwabudu yule msiyemjua, lakini sisi tunamjua huyo tunayemwabudu, kwa maana wokovu unatoka kwa Wayahudi.. 23 Lakini wakati waja, tena umekwisha wasili, ambapo wenye kuabudu wa kweli watamwabudu Baba katika roho na ukweli. Maana Baba anawataka watu wanaomwabudu namna hiyo. 24 Mungu ni roho, na watu wanaomwabudu lazima wamwabudu kwa Roho na ukweli.”
25 Huyo mama akamwambia, “Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu.”
26 Yesu akamwambia, “Mimi ninayeongea nawe, ndiye.”
27 Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?” 28 Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu, 29 “Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?” 30 Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.
31 Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: “Mwalimu, kula chakula.”
32 Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua nyinyi.”
33 Wanafunzi wake wakaulizana, “Je, kuna mtu aliyemletea chakula?”
34 Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake. 35 Nyinyi mwasema: ‘Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika!’ Lakini mimi nawaambieni, angalieni mkaone jinsi mashamba yalivyo tayari kuvunwa. 36 Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uhai wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja. 37 Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna.’ 38 Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho; wengine walifanya kazi, lakini nyinyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
39 Wasamaria wengi wa kijiji kile walimwamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.” 40 Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili. 41 Watu wengi zaidi waliamini kwa sababu ya ujumbe wake. 42 Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu.”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
11. Imani ya Ajabu
11. Imani ya Ajabu
Yohane 4:43-54
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Yohane 4:43-54
43 Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya. 44 Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, “Nabii hapati heshima katika nchi yake.” 45 Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
46 Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu. 47 Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
48 Yesu akamwambia, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!”
49 Huyo ofisa akamwambia, “Bwana, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa.”
50 Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao ataishi.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.
51 Alipokuwa bado njiani, watumishi wake walikutana naye, wakamwambia kwamba mwanawe alikuwa mzima. 52 Naye akawauliza saa mtoto alipopata nafuu; nao wakamwambia, “Jana saa saba mchana, homa ilimwacha.” 53 Huyo baba akakumbuka kwamba ilikuwa ni saa ileile ambapo Yesu alimwambia: “Mwanao ataishi.” Hapo yeye akaamini pamoja na jamaa yake yote. 54 Hii ilikuwa ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipokuwa anatoka Yudea kwenda Galilaya.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
12. Je, Unaamini Nini Kweli?
12. Je, Unaamini Nini Kweli?
Luka 4:14-30, Mathayo 4:18-22
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 4:14-30
14 Hapo Yesu alirudi Galilaya akiwa amejaa nguvu za Roho Mtakatifu, na habari zake zikaenea katika sehemu zote za jirani. 15 Naye akawa anawafundisha watu katika masunagogi yao, akasifiwa na wote.
16 Basi, Yesu alikwenda Nazareti, mahali alipolelewa, na siku ya Sabato, aliingia katika sunagogi kama ilivyokuwa desturi yake. Akasimama ili asome Maandiko Matakatifu kwa sauti. 17 Akapokea kitabu cha nabii Isaya, akakifungua na akakuta mahali palipoandikwa:
18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa, 19 na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana.”
20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho. 21Naye akaanza kuwaambia, “Andiko hili mlilosikia limetimia leo.”
22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”
23 Naye akawaambia, “Bila shaka mtaniambia msemo huu: ‘Mganga jiponye mwenyewe,’ na pia mtasema: ‘Yote tuliyosikia umeyafanya kule Kafarnaumu, yafanye pia hapa kijijini mwako.’” 24 Akaendelea kusema, “Hakika nawaambieni, nabii hatambuliwi kijijini mwake.
25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote. 26 Hata hivyo, Elia hakutumwa kwa mjane yeyote ila kwa mwanamke mjane wa Sarefathi katika Sidoni. 27 Tena, katika nchi ya Israeli nyakati za Elisha kulikuwa na wenye ukoma wengi. Hata hivyo, hakuna yeyote aliyetakaswa ila tu Naamani mwenyeji wa Siria.”
28 Wote waliokuwa katika lile sunagogi waliposikia hayo walikasirika sana. 29 Wakasimama, wakamtoa nje ya mji wao uliokuwa umejengwa juu ya kilima, wakampeleka mpaka kwenye ukingo wa kilima hicho ili wamtupe chini. 30 Lakini Yesu akapita katikati yao, akaenda zake.
Mathayo 4:18-22
18 Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani. 19 Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21 Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi, Yesu akawaita,. 22 nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
KIPINDI CHA 2 – MAISHA YA YESU
13. Wavuvi Wanne
13. Wavuvi Wanne
Mathayo 4:18-22, Marko 1:16-20
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Mathayo 4:18-22
Yesu Anawaita Wanafunzi Wake wa Kwanza
18 Yesu alipokuwa anatembea kando ya ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili wavuvi; Simoni (aitwaye Petro) na Andrea, ndugu yake; walikuwa wakivua samaki kwa nyavu ziwani. 19 Basi, akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya nyinyi wavuvi wa watu.” 20 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
21 Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wengine wawili: Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Hao walikuwa ndani ya mashua pamoja na baba yao Zebedayo, wakitengeneza nyavu zao. Basi, Yesu akawaita, 22 nao mara wakaiacha mashua pamoja na baba yao, wakamfuata.
Marko 1:16-20
16 Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu. 17 Yesu akawaambia, “Nifuateni nami nitawafanya nyinyi kuwa wavuvi wa watu.” 18 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19 Alipokwenda mbele kidogo, aliwaona Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo. Nao pia walikuwa ndani ya mashua yao wakizitengeneza nyavu zao. 20 Yesu akawaita mara, nao wakamwacha baba yao Zebedayo katika mashua pamoja na wafanyakazi, wakamfuata.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
14. Safari ya Kwanza ya Yesu ya Kuwavua Watu
14. Safari ya Kwanza ya Yesu ya Kuwavua Watu
Marko 1:21-28
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Marko 1:21-28
Yesu Anatoa Pepo Chafu
21 Wakafika mjini Kafarnaumu, na mara ilipofika Sabato, Yesu akaingia katika sunagogi, akaanza kufundisha. 22 Watu wote waliomsikia walishangazwa na mafundisho yake, maana hakuwa anafundisha kama waalimu wao wa sheria, bali kama mtu mwenye mamlaka. 23 Mara akatokea mle ndani ya sunagogi mtu mmoja mwenye pepo mchafu, 24 akapaza sauti, “Una nini nasi, wewe Yesu wa Nazareti? Je, umekuja kutuangamiza? Najua wewe ni nani: Wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”
25 Yesu akamkemea huyo pepo akisema, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu.” 26 Basi, huyo pepo mchafu akamtikisatikisa mtu huyo, kisha akalia kwa sauti kubwa, akamtoka.
27 Watu wote wakashangaa, wakaulizana, “Ni mambo gani haya? Je, ni mafundisho mapya? Mtu huyu anayo mamlaka ya kuamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!” 28 Habari za Yesu zikaenea upesi kila mahali katika eneo la Galilaya.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
15. Safari ya Pili ya Yesu ya Kuwavua Watu
15. Safari ya Pili ya Yesu ya Kuwavua Watu
Marko 1:29-39
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Marko 1:29-39
Yesu Anaponya Wengi
29 Wakatoka katika sunagogi, wakaenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Simoni na Andrea; Yakobo na Yohane walikwenda pamoja nao. 30 Basi, mama mmoja, mkwewe Simoni, alikuwa kitandani ana homa kali. Wakamwarifu Yesu mara alipowasili. 31 Yesu akamwendea huyo mama, akamshika mkono, akamwinua. Na ile homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
32 Jioni, jua lilipokwisha tua, wakamletea Yesu wagonjwa wote na watu waliopagawa na pepo. 33 Watu wote wa mji ule wakakusanyika nje ya mlango. 34 Naye Yesu akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali; aliwafukuza pepo wengi, lakini hakuwaruhusu kusema kitu maana walikuwa wanamjua yeye ni nani.
Yesu Anaomba Mahali pa Faragha
35 Kesho yake, kabla ya mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali. 36 Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta. 37 Walipomwona, wakamwambia, “Kila mtu anakutafuta.”
38 Yesu akawaambia, “Twendeni katika miji mingine ya jirani nikahubiri huko pia, maana nimekuja kwa sababu hiyo.” 39 Basi, akaenda kila mahali huko Galilaya akihubiri katika masunagogi na kufukuza pepo.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
16. Safari ya Tatu ya Yesu ya Kuwavua Watu
16. Safari ya Tatu ya Yesu ya Kuwavua Watu
Luka 5:1-11
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 5:1-11
Yesu Anawaita Wanafunzi Wake wa Kwanza
5 Siku moja, Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongamana, wanasikiliza neno la Mungu. 2 Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa. Wavuvi wenyewe walikuwa wametoka, wanaosha nyavu zao. 3 Baada ya Yesu kuingia katika mashua moja iliyokuwa ya Simoni, alimtaka Simoni aisogeze majini, mbali kidogo na ukingo wa ziwa. Akaketi, akafundisha umati wa watu akiwa ndani ya mashua.
4 Alipomaliza kufundisha, akamwambia Simoni, “Endesha mashua mpaka kilindini, mkatupe nyavu zenu mpate kuvua samaki.”
5 Simoni akamjibu, “Bwana, tumejitahidi kuvua samaki usiku kucha bila kupata kitu, lakini kwa kuwa umesema, nitatupa nyavu.”
6 Baada ya kufanya hivyo, wakavua samaki wengi, hata nyavu zao zikaanza kukatika. 7 Wakawaita wenzao waliokuwa katika mashua nyingine waje kuwasaidia. Wakaja, wakazijaza mashua zote mbili samaki, hata karibu zingezama.
8 Simoni Petro alipoona hayo, akapiga magoti mbele ya Yesu akisema, “Ondoka mbele yangu, ee Bwana, kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi!” 9 Simoni pamoja na wenzake wote walishangaa kwa kupata samaki wengi vile. 10 Hali kadhalika Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, waliokuwa wavuvi wenzake Simoni.
Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu.” 11 Basi, baada ya kuzileta zile mashua ukingoni mwa ziwa, wakaacha yote, wakamfuata.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
17. Safari ya Nne ya Yesu ya Kuwavua Watu
17. Safari ya Nne ya Yesu ya Kuwavua Watu
Luka 5:12-16
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 5:12-16
Yesu Anamponya Mtu Mwenye Ukoma
12 Ikawa, Yesu alipokuwa katika mmojawapo wa miji ya huko, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamwona. Basi, mtu huyo akaanguka kifudifudi akamwomba Yesu: “Bwana, ukitaka, waweza kunitakasa.”
13 Yesu akanyosha mkono, akamgusa na kusema, “Nataka! Takasika!” Mara ule ukoma ukamwacha.
14 Naye Yesu akamwamuru: “Usimwambie mtu yeyote; bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
15 Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. 16 Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
18. Safari ya Tano ya Yesu ya Kuwavua Watu
18. Safari ya Tano ya Yesu ya Kuwavua Watu
Luka 5:17-26
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 5:17-26
Yesu Anamsamehe na Kumponya Mtu Aliyepooza
17 Siku moja, Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na waalimu wa sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponya wagonjwa. 18 Mara watu wakaja, wamemchukua mtu mmoja aliyepooza maungo, amelala kitandani; wakajaribu kumwingiza ndani, wamweke mbele ya Yesu. 19 Lakini, kwa sababu ya wingi wa watu, hawakuweza kuingia ndani. Basi, wakapanda juu ya paa, wakaondoa vigae, wakamshusha huyo aliyepooza pamoja na kitanda chake, wakamweka mbele ya Yesu.
20 Yesu alipoona jinsi walivyokuwa na imani kubwa, akamwambia huyo mtu, “Rafiki, umesamehewa dhambi zako.”
21 Waalimu wa sheria na Mafarisayo wakaanza kujiuliza: “Nani huyu anayesema maneno ya kufuru? Hakuna mtu awezaye kusamehe dhambi ila Mungu peke yake!”
22 Yesu alitambua mawazo yao, akawauliza, “Mnawaza nini mioyoni mwenu? 23 Ni lipi lililo rahisi zaidi: Kusema, ‘Umesamehewa dhambi,’ au kusema, ‘Simama utembee?’ 24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.” 25 Mara, huyo mtu aliyepooza akasimama mbele yao wote, akachukua kitanda chake akaenda nyumbani kwake huku akimtukuza Mungu. 26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: “Tumeona maajabu leo.”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
19. Safari ya Sita ya Yesu ya Kuwavua Watu
19. Safari ya Sita ya Yesu ya Kuwavua Watu
Luka 5:27-32
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 5:27-32
Yesu Anamwita Lawi na Kula na Wenye Dhambi
27 Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtozaushuru mmoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, “Nifuate!” 28 Naye akaacha yote akamfuata.
29 Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake. Na kundi kubwa la watozaushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja nao. 30 Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanungunikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”
31 Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. 32 Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
20. Safari ya Sita ya Yesu ya Kuwavua Watu – Sehemu ya Pili
20. Safari ya Sita ya Yesu ya Kuwavua Watu – Sehemu ya Pili
Luka 5:36-39
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 5:36-39
36 Yesu akawaambia mfano huu: “Watu hawakati kiraka cha nguo mpya na kukitia katika vazi kuukuu; kama wakifanya hivyo, watakuwa wamelikata hilo vazi jipya, na pia hicho kiraka hakitachukuana na hilo vazi kuukuu. 37 Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; kwani hiyo divai mpya itavipasua hivyo viriba, divai itamwagika, na viriba vitaharibika. 38 Divai mpya hutiwa katika viriba vipya.. 39 Hakuna mtu anayetamani kunywa divai mpya baada ya kunywa divai ya zamani kwani husema ‘Ile ya zamani ni nzuri zaidi.’”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
21. Yesu Anachagua Kumi na Wawili
21. Yesu Anachagua Kumi na Wawili
Luka 6:12-19, Marko 3:13-19
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 6:12-19
Mitume Kumi na Wawili
12 Siku moja Yesu alikwenda mlimani kusali, akakesha huko usiku kucha akisali. 13 Kesho yake aliwaita wanafunzi wake, na miongoni mwao akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume: 14 Simoni (ambaye Yesu alimpa jina Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo na Yohane, Filipo na Bartholomayo, 15 Mathayo na Thoma, Yakobo wa Alfayo na Simoni (aliyeitwa Zelote), 16 Yuda wa Yakobo na Yuda Iskarioti ambaye baadaye alikuwa msaliti.
Baraka na Ole
17 Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao. 18 Aliwaponya pia wote waliokuwa wanasumbuliwa na pepo wachafu. 19 Watu wote walitaka kumgusa, kwa maana nguvu ilikuwa inatoka ndani yake na kuwaponya wote.
Marko 3:13-19
Yesu Anateua Kumi na Wawili
13 Yesu alipanda kilimani, akawaita wale aliowataka. Basi, wakamwendea, 14 naye akawateua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, wakae naye, awatume kuhubiri 15 na wawe na uwezo wa kuwafukuza pepo. 16 Basi, hao kumi na wawili walioteuliwa ndio hawa: Simoni (ambaye Yesu alimpa jina, Petro), 17 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo (Yesu aliwapa hawa ndugu wawili jina Boanerge, maana yake “Wanangurumo”), 18 Andrea na Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Thoma, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkanaani na 19 Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
22. Yesu Aliweka Matarajio
22. Yesu Aliweka Matarajio
Luka 6:20-49
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Luka 6:20-49
20 Yesu akawageukia wanafunzi wake, akasema: “Heri nyinyi mlio maskini, maana ufalme wa Mungu ni wenu.
21 Heri nyinyi mnaosikia njaa sasa, maana baadaye mtashiba. Heri nyinyi mnaolia sasa, maana baadaye mtacheka kwa furaha.
22 “Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.
23 Wakati hayo yatakapotokea, furahini na kucheza, maana hakika tuzo lenu ni kubwa mbinguni. Kwa maana wazee wao waliwatendea manabii vivyo hivyo.
24 Lakini ole wenu nyinyi mlio matajiri, maana mmekwisha pata faraja yenu.
25 Ole wenu nyinyi mnaoshiba sasa, maana baadaye mtasikia njaa. Ole wenu nyinyi mnaocheka kwa furaha sasa, maana baadaye mtaomboleza na kulia.
26 Ole wenu nyinyi iwapo watu wote wanawasifu, maana wazee wao waliwafanyia manabii wa uongo vivyo hivyo.
Upendo kwa Maadui
27 “Lakini nawaambieni nyinyi mnaonisikiliza, wapendeni maadui zenu, watendeeni mema wale wanaowachukieni. 28 Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 29 Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie pia la pili. Mtu akikunyanganya koti lako mwachie pia shati lako. 30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie. 31 Jinsi mnavyotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo.
32 “Na ikiwa mnawapenda tu wale wanaowapenda nyinyi, je, mtapata tuzo gani? Hakuna! Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wanaowapenda wao. 33 Tena, kama mkiwatendea mema wale tu wanaowatendeeni mema, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi hufanya hayo. 34 Na kama mnawakopesha wale tu mnaotumaini watawalipeni, je, mtapata tuzo gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi wenzao ili warudishiwe kima kilekile. 35 Ila nyinyi wapendeni maadui zenu na kuwatendea mema; kopesheni bila kutazamia kurudishiwa, na tuzo lenu litakuwa kubwa, nanyi mtakuwa watoto wa Mungu aliye juu. Kwa maana yeye ni mwema kwa wale wasio na shukrani na walio wabaya. 36 Muwe na huruma kama Baba yenu alivyo na huruma.
Kuhukumu Wengine
37 “Msiwahukumu wengine, nanyi hamtahukumiwa; msiwalaumu wengine, nanyi hamtalaumiwa; wasameheni wengine, nanyi mtasamehewa. 38 Wapeni wengine wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa, kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho atakachotumia Mungu kwenu.”
39 Akawaambia mfano huu: “Je, kipofu anaweza kumwongoza kipofu mwenzake? La! Wote wataanguka shimoni. 40 Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, lakini kila mwanafunzi akisha hitimu huwa kama mwalimu wake.
41 Kwa nini wakiona kibanzi jichoni mwa ndugu yako, na papo hapo huioni boriti iliyoko jichoni mwako? 42 Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.
Mti na Matunda Yake
43 “Mti mzuri hauzai matunda mabaya, wala mti mbaya hauzai matunda mazuri.. 44 Watu huutambua mti kutokana na matunda yake. Ni wazi kwamba watu hawachumi tini katika michongoma, wala hawachumi zabibu katika mbigili. 45 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.
Wajenzi Wenye Hekima na Wapumbavu
46 “Mbona mwaniita ‘Bwana, Bwana,’ na huku hamtimizi yale ninayosema? 47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza: 48 Huyo anafanana na mtu ajengaye nyumba, ambaye amechimba chini na kuweka msingi wake juu ya mwamba; kukatokea mafuriko ya mto, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, lakini haukuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa imara. 49 Lakini yeyote anayesikia maneno yangu asifanye chochote, huyo anafanana na mtu aliyejenga nyumba juu ya udongo, bila msingi. Mafuriko ya mto yakatokea, mkondo wa maji ukaipiga nyumba ile, ikaanguka na kuharibika kabisa!”
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
23. Chumvi na Nuru
23. Chumvi na Nuru
Mathayo 5:13-16
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Mathayo 5:13-16
13 “Nyinyi ni chumvi ya dunia. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake itakolezwa na nini? Haifai kitu tena, ila hutupwa nje na kukanyagwa na watu.
14 “Nyinyi ni mwanga wa ulimwengu! Mji uliojengwa juu ya mlima hauwezi kufichika. 15 Wala watu hawawashi taa na kuifunika kwa debe, ila huiweka juu ya kinara ili iwaangazie wote waliomo nyumbani. 16 Vivyo hivyo, ni lazima mwanga wenu uangaze mbele ya watu, ili wayaone matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
MATUMIZI / MAFUNZO
1. Sasa, hebu mtu mmoja asimulie kifungu hiki kwa maneno yake mwenyewe, kana kwamba anamhadithia rafiki ambaye hajawahi kukisikia.
2. Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu Mungu, tabia yake, na mambo anayofanya?
3. Tunajifunza nini kuhusu watu, wakiwemo sisi wenyewe, kutoka katika hadithi hii?
4. Utatumiaje ukweli wa Mungu kutoka katika hadithi hii katika maisha yako wiki hii? Ni kitendo au jambo gani maalum utakalofanya?
5. Ni nani utakayemshirikisha ukweli kutoka katika hadithi hii kabla hatujakutana tena? Je, unawajua wengine ambao pia wangependa kugundua Neno la Mungu kama sisi?
6. Tunapokaribia kumaliza mkutano wetu, hebu tuamue ni lini tutakutana tena na ni nani ataongoza mkutano wetu unaofuata.
24. Kuishi kwa Viwango vya Juu
24. Kuishi kwa Viwango vya Juu
Mathayo 5:17-48
UTANGULIZI
1. Kutokana na kile kilichokutokea tangu mara ya mwisho tulipokutana, ni jambo gani unaloshukuru kwa ajili yake?
2. Ni nini kimekusumbua wiki hii na unahitaji nini ili mambo yawe bora?
3. Sasa, hebu tusome hadithi ya leo kutoka kwa Mungu …
HADITHI
Mathayo 5:17-48
Utimilifu wa Sheria
17 “Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha. 18 Kweli nawaambieni, mpaka hapo mbingu na dunia zitakapopita, hakuna hata nukta moja au sehemu ndogo kabisa ya sheria itakayoondolewa, mpaka yote yametimia. 19 Basi, yeyote atakayevunja hata amri moja ndogo kuliko zote, na kuwafundisha wengine wafanye hivyo, huyo atakuwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni. Lakini yule atakayezishika na kuwafundisha wengine, huyo atakuwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. 20 Ndio maana nawaambieni, wema wenu usipozidi ule wa waalimu wa sheria na wa Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mauaji
21 “Mmekwisha sikia ya kuwa watu wa kale waliambiwa: ‘Usiue! Atakayeua lazima ahukumiwe.’ 22 Lakini mimi nawaambieni, yeyote anayemkasirikia ndugu yake, lazima ahukumiwe. Anayemdharau ndugu yake atapelekwa mahakamani. Anayemwita ndugu yake: ‘Pumbavu’ atastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
23 “Basi, ukipeleka sadaka yako mbele ya madhabahu na hapo ukakumbuka kwamba ndugu yako ana ugomvi nawe, 24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, nenda kwanza ukapatane na ndugu yako, ndipo urudi utoe sadaka yako.
25 “Patana na mshtaki wako upesi mkiwa bado njiani kwenda mahakamani. La sivyo, mshtaki wako atakukabidhi kwa hakimu, naye hakimu atakukabidhi kwa askari, nawe utafungwa gerezani. 26 Kweli nakuambia, hutatoka humo mpaka umelipa senti ya mwisho.
Uzini
27 “Mmesikia kwamba watu waliambiwa: ‘Usizini!’ 28 Lakini mimi nawaambieni, atakayemtazama mwanamke kwa kumtamani, amekwisha zini naye moyoni mwake.. 29 Basi, kama jicho lako la kulia linakukosesha, lingoe ukalitupe mbali. Afadhali zaidi kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote kutupwa katika moto wa Jehanamu. 30 Na kama mkono wako wa kulia unakukosesha, ukate ukautupe mbali. Afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako, kuliko mwili wako wote uende katika moto wa Jehanamu.
Talaka
31 “Ilikwisha semwa pia: ‘Anayemwacha mke wake, yampasa ampe hati ya talaka’. 32 Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Viapo
33 “Tena mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa: ‘Usivunje kiapo chako, bali ni lazima utimize kiapo chako kwa Bwana.’ 34 Lakini mimi nawaambieni, msiape kamwe; wala kwa mbingu, maana ni kiti cha enzi cha Mungu; 35 wala kwa dunia, maana ni kiti chake cha kuwekea miguu; wala kwa Yerusalemu, maana ni mji wa Mfalme mkuu. 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kuufanya hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema, ‘Ndiyo’, basi iwe ‘Ndiyo’; ukisema, ‘Siyo’, basi iwe kweli ‘Siyo’. Chochote kinachozidi hayo hutoka kwa yule Mwovu.
Jicho kwa Jicho
38 “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili. 40 Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako. 41 Mtu akikulazimisha kubeba mzigo wake kilomita moja, ubebe kilomita mbili. 42 Akuombaye mpe, wala usimpe kisogo anayetaka kukukopa kitu.
Upendo kwa Maadui
43 “Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Mpende jirani yako, na kumchukia adui yako.’ 44 Lakini mimi nawaambieni, wapendeni maadui zenu na kuwaombea wale wanaowadhulumu nyinyi, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu wabaya na wema, na kuwanyeshea mvua watu wanyofu na waovu. 46 Je, mtapata tuzo gani kwa kuwapenda tu wale wanaowapenda nyinyi? Hakuna! Kwa maana, hata watozaushuru hufanya hivyo! 47 Kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mmefanya kitu kisicho cha kawaida? Hata watu wasiomjua Mungu nao hufanya vivyo hivyo. 48 Basi, muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.